Halima Mdee afunguka kuungana na Zitto Kabwe
Baada ya Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe kuomba kuunganisha nguvu ya pamoja na CHADEMA ili kufanikisha kuing'oa CCM kwenye chaguzi ndogo za madiwani, Halima Mdee amefunguka na kusema kwamba hatoshangaa chama chake kushirikiana na ACT Wazalendo.
Halima Mdee ambaye ni Mbunge wa Kawe kupitia CHADEMA ameyasema hayo alipokuwa akiongea na mwandishi wa East Africa Television, na kueleza kwamba wao kama wanasiasa wanaangalia ni namna gani wanaweza kufikia lengo kwa pamoja, hivyo sio mbaya kama wataungana na ACT Wazalendo kufanikisha mambo ambayo wao pia wanayapigania.
Halima Mdee ameendelea kwa kusema kwamba sasa hivi ana imani na kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ambaye alifukuzwa kwenye chama hicho wakimuita msaliti, na kwamba kiongozi huyo sasa anarudi kwenye mstari ambao unamfaa.
Post a Comment