Wakongo kuhesabiwa Tanzania
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania amewataka wananchi wenye asili ya Congo wanaoishi Tanzania kutembelea ubalozi huo ili waweze kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura wakati wa Uchaguzi wa rais wa nchi ya Congo kwani kura zao pia zitahesabiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo balozi wa Congo nchini Ndg, Balozi Jean Pierre Mutamba amesema wameshakutana na Wapinzani pamoja na Chama tawala ili kujadili namna ya kuuwezesha uchaguzi huo ufanyike kwa amani.
Aidha Balozi Mutamba ameeleza kuwa serikali ni moja hata kama kuna makundi ya upinzani ila kinachotakiwa ni Wapinzani kuteua watu maalumu watakao shiriki uchaguzi huo.
Hata hivyo amefafanua kuwa hadi sasa wameshafikisha mapendekezo yao kwa rais wa sasa ya kumuomba uchaguzi ufanyike kwa amani.
Aidha uchaguzi huo wa Congo unatarajiwa kufanyika September 23, 2018 ambapo uchaguzi huo utakuwa ni wa Serikali ya awamu ya tatu.
Post a Comment