RC MAKONDA AFURAHISHWA NA KASI YA MATIBABU YA BURE NDANI YA MELI YA KICHINA !

Zoezi la Upimaji wa Afya na Matibabu Bure Ndani ya *Meli ya Jeshi la Jamuhuri ya Watu wa China* Leo limeingia Siku ya Pili ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam *Mhe. PAUL MAKONDA*amesema Wagonjwa ambao wataonekana kuwa na Hali mbaya *watasafirishwa kutibiwa Bure Nchini China*. 
*RC MAKONDA* amesema Ofisi yake itaratibu utaratibu wa *Hati za Kusafiria* (Passport) ili kuhakikisha Wagonjwa wanapatiwa Matibabu ili *kuokoa Maisha yao.* 
Aidha amesema Wagonjwa Wanaopangiwa kulazwa kwenye Meli hiyo yenye *Vitanda vya Wagonjwa zaidi ya 300* wanapatiwa huduma za *Malazi Bure ikiwemo Chakula, Vinywaji, Mavazi.*
Aidha *RC MAKONDA* amekemea tabia ya baadhi ya Watu *wanaochuchuwa Kadi za Matibabu kisha kuziuza kwa Watu.* 

*MAKONDA* amesema kasi ya utoaji wa huduma  ni nzuri hivyo anaamini *hadi siku ya Mwisho ya Zoezi la Upimaji Wananchi wote waliopatiwa namba watakuwa wamehudumiwa.* 
Katika kuongeza nguvu kasi ya Upimaji *Madaktari kutoka JWTZ,  Muhimbili na Hospital za mkoa wa Dar es salaam Ikiwemo Amana,  Temeke na Mwananyamala* wanashirikiana na Madaktari wa China katika kutoa huduma.