Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameamuru wahamiaji raia wa Nigeria waliokwama nchini Libya na mahali pengine duniani warejeshwe nyumbani.


Uamuzi wa Rais Buhari umekuja kufuatia picha za video zilizosambazwa zikionyesha wahamiaji wakiuzwa kama watumwa katika mnada nchini Libya.
Rais Buhari amesema watu hao wamekuwa wakifanywa kama mbuzi na kuapa kuwa atafanya kila awezalo kuzuia raia wengine wa Nigeria kufanya ziara za kwenda ulaya.
Tangazo hilo limetolewa baada ya mamlaka inayoungwa mkono na umoja wa mataifa ya Libya kusema kwamba inaongeza idadi ya ndege ya kuwarejesha makwao wahamiaji walioko nchini Libya ambao wamekwama.
Takribani wahamiaji 240 raia wa Nigeria kwa utashi wao waliamua kurejea kwao chini ya usimamizi wa serikali ya Libya na wakala wa umoja wa mataifa wa wahamiaji siku ya Jumanne usiku.