Lukuvi aagiza kukamatwa kwa wanasheria

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ameliagiza Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kuwakamata baadhi ya maafisa ardhi na baadhi ya wanasheria ambao wamehusika katika uuzaji wa shamba kiasi cha Hekta mbili na nusu mali
ya Madina Omary Mkazi wa Bagamoyo mkoani Pwani.
Mhe Lukuvi ametoa kauli hiyo akiwa ofisi kwake mkoani Dodoma mbele ya waandishi wa habari wakati akimrejeshea mama huyo ardhi yake huku akiwataka maafisa ardhi na wanasheria kufuata taratibu zote za uuuzaji wa ardhi wakati wa kuuza.
Mhe Lukuvi amesema uuzaji wa shamba hilo ulikiuka taratibu za uuzaji wa eneo hilo ikiwemo kuwepo kwa sahihi za kufoji za wahusika wa shmba hilo huku mawikili waliofanya hivyo wakijua kuwa hilo ni kosa kisheria.
Kwa upande wake mama huyo Madina Omary amemshukuru Mhe Waziri Lukuvu kwa kumsaidia kupata ardhi hiyo ambayo alikua amedhulumiwa kwa zaidi ya miaka kumi kutoka kwa matepeli ambao alikua akishindana nao mahakamani