Wema atia neno kuhusu Lissu na Nyalandu

Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu amefunguka na kuweka wazi kuwa anajisikia furaha na amani kuona Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kuwa anaendelea vyema kadili siku zinavyokwenda lakini pia amegusia sakata la Nyalandu kujitoa CCM. 

Wema Sepetu ametumia mtandao wake wa Instagram baada ya kuweka picha ya Tundu Lissu akiwa anakula chakula akiwa hospitali Nairobi na kusema anajisikia vizuri kuona shujaa wao anaendelea vizuri. 

"Ni jambo jema kumuona shujaa wetu anaendelea vyema kweli Mungu ni mwema siku zote, lakini pia nikiwa mkubwa nitahitaji kuwa kama Lazaro Nyalandu" aliandika Wema Sepetu 


Wema Sepetu ameweka ujumbe huu masaa kadhaa toka Lazaro Nyalandu alipotangaza kujivua uanachama wake ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuandika barua kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge wa Singida Kaskazini na kuomba kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)