LEMA:Tutaandika barua kwa DCI - Lema
Mbunge wa Arusha Mjini kupitia CHADEMA Godbless Lema, amesema wanakusudia kuandika barua maalum kwa DCI ili kutoa taarifa dhidi ya vitisho wanavyopata vinavyohatarisha maisha yao.
Godbless Lema ameyasema hayo alipokuwa akiongea na mwandishi wa East Africa Television kwa njia ya simu mara baada ya tukio la gari lake kutolewa nati za matairi ya gari, na kusema mashaka hayo yanahatarisha maisha yao na kuyafanya kuwa magumu kwao na familia zao, hivyo wataripoti kwa DCI waweze kupatiwa msaada.
Pamoja na hayo Godbless Lema amesema wana taarifa nyeti wanazozipata kutoka kwa intelijensia yao, na muda ukifika kila kitu wataweka wazi.
Post a Comment