Wabunge wamsusia Rais
Wabunge wa upinzani nchini Kenya wamesusia uzinduzi wa bunge la nchi hiyo, uliofanyika leo mchana, baada ya Rais Uhuru Kenyata kuhutubia kupitia bunge hilo.
Taarifa zinasema kuwa wabunge hao wamefikia uamuzi huo na kusema Uhuru Kenyata hana mamlaka ya kuhutubia bunge, mpaka pale uchaguzi wa marudio utakapofanyika Oktoba 17, 2017 na badala yake waliamua kuendelea na kampeni za urais za mgombea wao Raila Odinga
Kwa upande wa Uhuru Kenyatta amesema bado ana mamlaka ya kuhutubia bunge hilo kama Rais wa Kenya, na kufanya hivyo mara baada ya bunge hilo kuzinduliwa.
Septemba 1 mwaka huu Mahakama ya Juu nchini Kenya ilitengua ushindi wa Uhuru Kenyata kwa kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais, na kutaka uchaguzi huo urudiwe.
Post a Comment