Hili ni pigo- Manara
Afisa habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara ameguswa na taarifa ya kifo cha mlinda
mlango wa timu ya Rayon Sports kutokea nchini Rwanda, Evariste Mutuyimana na
kusema hilo ni pigo kubwa sana kwa klabu yake na wapenda soka.
Afisa habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara. |
Manara ametoa salamu hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram muda mchache baada ya taarifa za kifo cha mchezaji huyo zilipoenea kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.
"Ni pigo kubwa sana kwa Rayon ya Rwanda, kipa huyu alidaka dhidi yetu kwenye Simba Day. Klabu yetu inawapa pole Rayon na Wanyarwanda wote, Mungu pekee ndiyo mpangaji wa haya yote. RIP Mutuyimana Evariste", ameandika Manara
Post a Comment