POLISI: DEREVA WA TUNDU LISSU TUNAMSAKA, TUMEKAMATA MAGARI 30 MPAKA SASA


Polisi Dodoma limekamata magari 8 na aina ya Nissan Patrol kwa ajili ya uchunguzi wa tukio la kupigwa kwa risasi Tundu Lissu, RPC Muroto asema

Pia jeshi hilo linaendelea kutoa wito kwa wananchi walio taarifa kuwapa ushirikiano ili kuwarahisishia kazi

Amesema tokea tukio la kushambuliwa kwa mbunge huyo dereva wake ajulikanaye kwa jina la Adam bado hajaonekana ila ameona mahojiano yake kwenye gazeti la Mtanzania na kutoa wito kuwa afike ofisi ya mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Dodoma au ofisi ya mkurugenzi wa makosa ya jinai Dar kwa kuwa wanaamini ana taarifa za siri na kutofika kwake kutawapa mashaka kwamba kuna jambo anaficha

Na sheria kifungu cha 9 na 10 kidogo sehemu ya 2 inasema mtu mwenye taarifa kuhusiana na uhalifu na akakataa kuwapa polisi taarifa hizo atakuwa anatenda kosa la jinai

Pia amesema jeshi la polisi ndilo lenye mamlaka pekee ya kufanya uchunguzi kwenye makosa yote ya jinai na limemekwa na mamlaka na kumtaka Katibu mkuu wa Chadema Vincent Mashinji aliyekuwa akisema anawafahamu waliofanya shambulio hilo kufika ofisi ya mkuu wa upelelezi Dodoma au mkurugenzi wa makosa ya jinai Dar kuwapa maelezo

Pia amesema jeshi lisiingiliwe na tukio hilo lisipelekwe kisiasa na kuchochea wananchi kuichukia serikali yao, matukio mengi yametokea na polisi wamefanikisha kupata wahalifu akitolea mfano matukio ya Kibiti na Mbande na Kongowe ambapo polisi walipoteza maisha

Watuhumiwa wengine 30 wamekamatwa kwa matukio mbalimbali ikiwemo kukutwa na bangi na pombe aina ya gongo
[​IMG]
Chanzo: Mwananchi