Breaking: Bodaboda wamshambulia vikali dereva wa daladala Dar




Boda boda wanaofanya shughuli zao maeneo ya Ubungo, leo wamemshambulia dereva wa gari aina Coaster lililokuwa likitokea maeneo ya Ubungo baada ya kumgonga boda boda maeneo hayo. Aidha, baada ya kutokea kwa ajali hiyo dereva hakutaka kusimama ndipo boda boda hao walianza kumfukuza huku wakipiga honi wakiashiria kuwa ni mwizi. Hata hivyo, boda boda hao walifanikiwa kumpata dereva huyo maeneo ya Magomeni na kuanza kumshambulia na kumsababishia majeraha makubwa ambayo yalimfanya kupoteza fahamu, mpaka alipokuja kuokolewa na askari Polisi waliokuwa karibu na eneo hilo.