Nyalandu akomaa na Tundu Lissu
Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu (CCM) amendelea kushika bango sakata la Tundu Lissu kwa kuhamasisha wananchi kwenye mitandao ya kijamii kuweza kuchangua gharama za matibabu ili Tundu Lissu aweze kupatiwa matibabu hospitali mahiri duniani
Lazaro Nyalandu amezidi kuwaomba Watanzania wote kumkumbuka Mbunge huyo kwa sala na dua wakati huu ambao amepata majaribu hayo na kuendelea kuwasisitiza kuchangia fedha kwa ili mbunge huyo apatiwe matibabu bora zaidi.
"Tunawaomba wana Singida na Watanzania wote tuendelee kuchangia gharama za matibabu ya Mhe. Tundu Lissu sote tumkumbuke katika sala na dua zetu katika majira ya saa hii ya kujaribiwa kwake. Mungu akisema ndio, hakuna awezaye kupinga. Kwa wote wanaohusika moja kwa moja kumtibu na kumtunza, mikozo yao na fahamu zao zikahuishwe katika ubora wote wa utabibu na matunzo" alisema Nyalandu
Aidha Mbunge huyo aliendelea kusema kuwa anaomba mazungumzo yanayoendelea na madaktari bingwa na hospitali mahiri yakafanikiwe kwa haraka ili kiongozi huyo akapatiwe matibabu na huduma bora zaidi ulimwenguni.
"Mazungumzo yanayoendelea na madaktari bingwa na hospitali mahiri kote duniani yafanikiwe upesi kumwezesha Mh. Lissu kuifikia huduma bora ya matibbu iliyopo kwa sasa ulimwenguni" alisema Nyalandu.
Kufuatia kuonyesha moyo wa upendo na utu kwa Mbunge huyo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwanza kufunga safari mpaka nchini Kenya kumjulia hali Tundu Lissu na kuzidi kushawishi watu kuchangia michango ili mbunge huyo akapate matibabu na huduma bora zaidi, wananchi wamempongeza sana Nyalandu kwa moyo wake huo huku wengine wakisema wamejifunza jambo kupitia yeye.
Post a Comment