Milioni 5 sio kitu kwa ndoa - Gigy Money

Msanii Gigy Money ambaye kila kukicha hakauki midomoni mwa watu kutokana na vituko vyake, ametoa sababu ya kukataa kuolewa na kukimbia kabisa ndoa kwa mahari ya milioni 5, na kusema pesa hiyo haikuwa kitu kwake.
Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Gigy Money amesema mahari hiyo haikuwa sababu ya yeye kukataa ndoa, isipokuwa hana mapenzi na huyo aliyemtengazia ndoa.
"Nilikataa kwa sababu ilikuwa ni njia ya kumkataa tu yule mtu, sio ndogo hiyo hela, nilikuwa simtaki, nikataja hela nyingi zaidi basi akashindwa, sikuwa nampenda ningemtesa tu", amesema Gigy Money.
Pamoja na hayo Gigy Money ameendelea kusema kwamba kwa mtu ambaye anahitaji kumuoa amuandalie tu mazingira ya kuwa mke, lakini cha muhimu ataangalia upendo