Kipa aliyedaka mechi ya Simba Day afariki

Golikipa wa Rayon Sports, Evariste Mutuyimana aliyedaka kwenye mechi dhidi ya Simba siku ya Simba Day jijini Dar es Salaam katika uwanja wa Taifa , amefariki dunia leo Jumanne kwenye Hospitali ya Kigali nchini Rwanda.
Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA) limethibitisha kutokea kwa kifo cha mchezaji 
huyo, 
huku likitoa salamu za pole kwa klabu ya Rayon Sports.
Mchezaji huyo alijiunga na klabu hiyo msimu wa mwaka 2016/17
 akitokea Sofapaka  ya Kenya.