Halima Mdee alivimbia jeshi la Polisi
Mbunge wa jimbo la Kawe jijini Dar es salaa Halima James Mdee amesema hajaenda kuripoti kwa DCI kama ilivyotakiwa kwa sababu yeye hajaitwa rasmi.
Halima Mdee |
Akizungumza na mwandishi wa habari wa East Africa Television Halima Mdee amesema DCI ametoa tangazo la ujumla, lakini yeye binafsi hajapewa wito wowote, hivyo hawezi kwenda kutokana na taarifa hiyo.
"Mimi nimesikia tangazo la ujumla, wakiniita in personel Halima njoo nitaenda na hakuna popote kwenye kauli yao iliposema Halima Mdee njoo, lakini siwezi kwenda kwa 'general statement', amesema Halima Mdee
Juzi Jeshi la Polisi liliwataka watu wote waliopost kwenye mitandao ya kijamii kuhusu askari wao aliye nchini Nairobi wakimuhusisha na kumfuatilia Tundu Lissu nchini Kenya kwenye matibabu na kutakiwa kuripoti wenyewe kwa DCI, kabla ya kitengo cha sheria za makosa ya mtandaoni hakijawachukulia hatua zaidi.
Post a Comment