DC ASIA APIGA MARUFUKU WILAYA YA KILOLO KUTOA WAFANYAKAZI WA KAZI ZA NDANI.

Mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah akiwa katika moja ya shule za msingi wilayani kilolo akiwa amefika kaunagalia hali ya mitihani inaendeshwani na usalama wake upoje 
 Mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah akizungumza na wanafuzi waliohitimu elimu ya shule ya msingi katika shule ya msingi Boma la ng’ombe wilaya kilolo mkoani Iringa 
Na fredy Mgunda,Iringa.
Wananchi
wa wilaya ya kilolo mkoani iringa watafungwa kwa kuwapeleka watoto wao kufanya
kazi za ndani pindi wamemalizapo shule ya msingi au sekondari kufanya hivyo
kunadumaza uchumi wa taifa.
 
Akizungumza
wakati wa kuangalia amani ya wanafunzi wa darasa la saba waliokuwa wanafanya
mitihani ya kuhitimu elimu ya shule ya msingi mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah
alisema sasa imefika mwisho wa wilaya hiyo kuwa soko la wafanyakazi wa ndani.
 
“Nasema
tena haiwezekani kila mfanyakazi ukifika daresalaam utasikia katoka iringa
kilolo sasa sitaki kusika swala hilo na wazazi wanaofanya hivyo nitawakamata na
kuwafungulia kesi serikali ya awamu ya tano inataka kuwa na wasomi wengi ili
kuasaidia maendeleo ya nchi”alisema Abdallah
 
Abdallah
aliwataka wananchi wa wilaya hiyo kuwapeleka shule watoto waliofaulu kinyume
cha hapo wazazi watachukulia hatua kali.
 
“Haiwezekani
mwanafunzi amefaulu halafu mzazi anampeleka kufanya kazi za ndani siwezi
kukubari hata kidogo maana nimegundugua wazazi wengi hawapendi watoto wao
waendelee kusoma badala yake wanataka wakafanye kazi za ndani narudia kusema
mtoto akifaulu asipopelekwa shule nitamchulia hatua za kisheria huyo mzazi”
alisema Abdallah
 
Aidha
Abdallah aliwataka wanafunzi wakike kuacha kufanya ngono wakiwa na umri mdogo
ili kupunguza mimba za utotoni na kupoteza dira ya maisha wakiwa watoto wadogo.
“Acheni
kuwavulia chupi wanaume mkiwa na umri mdogo ili baadae mjenge maisha yetu kama
mimi ambavyo leo hiii nimekuwa kiongozi wenu kwa kwasababu nilikataa kuvua
chupi nikiwa na umri kama wenu ndio maana leo hii nipo hapa”alisema Abdallah
 
Aidha
Abdallah aliwapongeza walimu wa shule za msingi za wilaya ya kilolo kwa
kuendelea kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa na kuendelea kuitangaza
vizuri wilaya ya kilolo kupitia elimu.
 
“Kwa
kweli nisiwe mnafiki nichukue fursa hii kuwapongeza walimu wa wilaya hii kwa
kufanya vizuri maana kila mwaka elimu inazidi kukua katika wilaya yangu ya
kilolo na kuendelea kuitangaza kitaifa” alisema Abdallah
 
Kwa
upande wake diwani wa kata ya boma la ng’ombe Anderson Mdeke alikiri kuwepo kwa
tatizo la mimba shuleni limekuwa sugu hivyo wameanza kuridhibiti na limepungua
kwa kiasi kikubwa.
 
“Kwa
kweli tatizo la mimba kwenye shule za kata yangu ya lipo na tumeanza kutafutia
ufumbuzi ili kulikosesa kabisa ili watoto wetu wasome bila kuwa na buguza”
alisema Mdeke
 
Naye mwalimu wa shule ya msingi Mwanzala Grace Magawa alikiri
kuwepo kuwepo kwa mimba za utotoni katika
baadhi ya shule za msingi za wilaya ya kilolo kutokana mazingira
yanayowakabili baadhi ya wanafunzi ndio husababisha mimba za utoto.
 
“Mwanafunzi akirudi nyumbani anawakuta wazazi wake
washakunywa pombe na hawana habari ya kuulizia maendeleo ya mtoto wake hivyo mtoto
anaamua kufanya anachotaka kutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha kutoka kwa
wazazi wake au walezi wake” alisema Magawa