Waendesha bodaboda 3 Kenya wauawa na al-Shabaab
Waendesha pikipiki watatu, maarufu kwa jina la bodaboda, wameuawa na
shambulizi linaloshukiwa limefanywa na al-Shabaab katika eneo la Witu,
kwenye Kaunti ya Lamu, Kenya.
Watu hao watatu walikufa baada ya mtu mwenye silaha kurusha risasi
kwenye basi na gari la kampuni ya ulinzi lililokuwa linaelekea huko eneo
la Kipini kutoka mji wa Malindi.
Washambuliaji hao walilitupia risasi basi ambalo ni mali ya kampuni
ya Kipini Raha katika barabara kuu ya Garsen-Lamu katika mida ya saa
3.30pm, kwa mujibu walioshuhudia tukio hilo..
Wapiganaji hao walitupa risasi kila upande kutoka porini kabla ya
polisi waliokuwa wanalisindikiza gari hilo kuja haraka kuwaokoa watu
waliokuwa wanasafiri katika basi hilo.
Vyanzo vya habari vimesema kuwa kuna wasafiri ambao idadi yao
haijajulikana waliokuwa wamejeruhiwa na walipelekwa hospitali ya Kaunti
ndogo huko Witu.
Mkurugenzi Joseph Kanyiri aliyechaguliwa kusimamia operesheni hiyo ya
Linda Boni amethibitsha kutokea shambulizi hilo lakini amesema bado
anasubiri taarifa zaidi juu ya shambulizi hilo.
Post a Comment