WADAU WAENDELEA KUUNGA MKONO JITIHADA ZA RC MAKONDA
Posted on: August 2nd, 2017
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo amepokea Jumla ya Computer za kisasa 100 zenye thamani ya Shilingi Million 210 kutoka kiwanda cha utengenezaji wa nguo zitokanazo na pamba ya Tanzania cha NIDA Textile Ltd.
Makonda amesema Computer hizo atazitoa kwa Vituo vya Polisi 20 kwaajili ya kufungwa mfumo wa kisasa wa kuripoti taarifa za uhalifu zilizoripotiwa kwenye Vituo vya Polisi kila siku (Crime Statistic Management Information System) kupambana na uhalifu.
Faida za Mfumo ni kumsaidia Mwananchi kupata taarifa za ndugu yake
aliepotea pasipokujua yupo wapi kwa kumuangalia kwenye mfumo kama
anashikiliwa kwenye Kituo cha Polisi mfumo utaonyesha taarifa zake kwa
wakati kwenye kila Kituo.
Aidha mfumo utasaidia viongozi kupata taarifa za uhalifu
zinazoripotiwa katika vituo vya Polisi kwa wakati na kupunguza uhalifu
kwani taarifa zote za wahalifu zitaonekana kuanzia ngazi ya Mkuu wa
Mkoa, Kamanda wa Mkoa,Wilaya na Mkuu wa kituo hivyo kusaidia viongozi
kufanya maamuzi.
Mfumo pia utaondoa Rushwa na matukio ya Wananchi kubambikiziwa kesi
kwani kila atakaefikishwa kituo cha Polisi viongozi wote akiwemo
Mheshimiwa Makonda atapata kujua.
Mfumo pia utamuwezesha kiongozi kujua idadi na aina ya uhalifu
unaofanyika kwa siku,eneo ambapo matukio hujirudia mara kwa mara sanjari
na mhalifu ambae matukio yake ya uhalifu yamekuwa yakijirudia maeneo
mbalimbali.
“Tunaachana na kuandika taarifa kwenye makaratasi na
makaunta au madaftari kwenye Vituo vya Polisi ambayo baada ya muda mfupi
yanapotea na kumuacha Mwananchi hajui kesi yake imeishia wapi, huu
mfumo ni ukombozi na mwonekano mpya wa Jeshi la Polisi na hata Wananchi
wataachana na matatizo ya rushwa na watu kubambikiziwa kesi” Alisema Makonda.
Mfumo wa CSMIS utachukuwa taarifa za Mhalifu kuanzia
anapoingia kituo cha polisi CRO, Jina la Mhalifu, Aina ya kesi,jina la
Mpelelezi, Hakimu, Mahakama anayopelekwa na kama amehukumiwa kulipa
faini au kifungo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kiwanda cha NIDA Bwana
Mohamed Hamza amesema kampuni yao imeamua kuunga mkono jitiada za
Mheshimiwa Makonda katika dhamira yake ya kufanya Mabadiliko ya mfumo wa
utendaji kazi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam.
Post a Comment