TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA
taarifa ya jeshi la polisi mkoa wa mwanza kwa
vyombo
vya habari leo tarehe 10.08.2017
·
watu
wawili wamefariki dunia na mwingine mmoja kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha
gari na bajaji wilayani kwimba.
·
mtu
mmoja anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kupatikana na noti bandia za
elfu kumi 20 zenye thamani ya tsh 200,000/=, wilayani sengerema.
kwamba tarehe 09.08.2017 majira ya saa 21:00hrs
katika barabara ya ngudu kwenda hungumalwa eneo la kitongoji cha mwalugunda
kijiji na kata ya nyamilama wilaya ya kwimba mkoa wa mwanza, gari namba
t.355 arz aina ya mistubishi fuso likitokea ngudu kwendwa hungumalwa
likiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la muro robart, miaka 35, mkazi
wa mkoa wa kilimanjaro liligonga bajaji ya magurudumu matatu yenye namba t.675
buf iliyokuwa ikitokea hungumalwa kwenda ngudu ikiendeshwa na dereva aitwaye
kulwa philimon @ fulano miaka 50, mkazi wa kijiji cha nhaniga, na kusababisha
vifo kwa 1.kulwa philimon @ fulano dereva bajaji, 2.jina bado halijafahamika,
abiria wa bajaji, na kusababisha majeruhi kwa edward dornad miaka 42, abiria wa
bajaji, mfanyabiashara, mkazi wa nyamilama.
inadaiwa kuwa majira tajwa hapo juu dereva wa
bajaji alikuwa akitokea maeneo ya hungumalwa akielekea ngudu huku akiwa amebeba
abiria wawili lakini bajaji yake ilikuwa haina taa na kutokana na bajaji
hiyo kukosa taa dereva wa bajaji hiyo inasemekana alikuwa akitumia tochi
aliyokuwa ameifunga kifuani kama taa, ndipo alipofika eneo hilo tajwa hapo juu
dereva wa gari alishindwa kutambua ujio wa bajaji na kupelekea kugongana na
kusababisha vifo vya watu wawili tajwa hapo juu na majeruhi, ambapo dereva wa
gari baada ya jali kutokea alitoroka eneo la tukio, juhudi za kumtafuta bado
zinaendelea.
uchunguzi wa awali unaonesha chanzo cha ajali ni
uzembe wa dereva wa bajaji kuendesha chombo cha moto barabarani bila ya taa
na kupelekea ajali hiyo kutokea na kupelekea vifo na majeruhi. majeruhi
amelazwa hospitali ya wilaya ya ngudu akiendelea kupatiwa matibabu na hali yake
inaendelea vizuri, miili ya marehemu pia imehifadhiwa hospitalini hapo kwa
ajili ya uchunguzi, pindi uchunguzi ukikamilika itakabidhiwa kwa ndugu wa
marehemu kwa ajili ya mazishi.
kamanda wa polisi mkoa wa mwanza naibu kamishina
wa polisi ahmed msangi anatoa wito kwa wakazi wa jiji na mkoa wa mwanza
hususani waendeshaji wa vyombo vya moto akiwataka kuchukua tahadhari pindi
wawapo barabarani huku wakizingatia sheria, kanuni na taratibu za usalama
barabarani ili kuepusha ajali na vifo vinavyoweza kuepukika.
katika tukio la pili,
mnamo tarehe 09.08.2017 majira ya saa 14:00hrs
katika kijiji cha kanyara kata ya bulyaheke tarafa ya buchosa wilaya ya
sengerema mkoa wa mwanza, fabian jackson miaka 32, mkazi wa mahina mwanza,
anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kupatikana akiwa na noti bandia 20
za elfu kumi zenye thamani ya kiasi cha tsh 200,000/=, kitendo ambacho ni kosa
la jinai.
awali polisi wakiwa kwenye doria na misako
walipokea taarifa kwamba katika kijiji cha kanyara yupo mtu ambae ameingia
kijijini hapo lakini ana noti bandia nyingi. aidha baada ya askari kupokea
taarifa hizo walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi kijijini hapo na kufanya
upelelezi na msako wa kumtafuta mtu huyo
ndipo baadae walifanikiwa kumtia nguvuni
mtuhumiwa akiwa na kiasi hicho tajwa hapo juu cha noti hizo bandia.
polisi wapo katika upelelezi na mahojiano na
mtuhumiwa kuhusiana na tukio hilo pindi uchunguzi ukikamilika mtuhumiwa
atafikishwa mahakamani. aidha msako wa kuwatafuta watu wengine wanaoshirikiana
na mtuhumiwa katika utengenezaji wa noti bandia bado unaendelea.
kamanda wa polisi mkoa wa mwanza naibu kamishina
wa polisi ahmed msangi anatoa rai kwa wakazi wa mkoa wa mwanza, akiwataka
kuacha tabia ya kutengeneza noti bandia kwani ni kosa la jinai na endapo mtu
akikamatwa hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. aidha pia
anaendelea kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuweza
kudhibiti uhalifu katika mkoa wetu.
imetolewa na;
dcp: ahmed msangi
kamanda wa polisi (m) mwanza
Post a Comment