Msajili wa Vyama vya Siasa Apinga Maamuzi ya CUF.....Kasema Hamtambui Maalim Seif Kama Katibu Mkuu CUF
Msajili
wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amepinga maamuzi ya
Chama Cha Wananchi (CUF) kuwafukuza Uanachama Wabunge wawili wa chama
hicho Magdalena Sakaya na Maftaha Nachuma na kusema Maalim Seif
hatambuliki kama Katibu Mkuu wa CUF.
Msajili
wa Vyama vya Siasa amesema hayo leo wakati akijibu barua
iliyowasilishwa ofisini kwake na Katibu Mkuu wa (CUF) Maalim Seif Sharif
Hamad akimtaka msajili wa vyama kuwavua nafasi ya Ubunge viongozi hao.
Kufuatia
barau hiyo Msajili wa Vyama Vya Siasa amesema kuwa hamtambui Maalim
Seif Sharif Hamad kama Katibu Mkuu wa CUF na kusema yeye anawatambua
Mwenyekiti wa CUF, Professa Ibrahim Lipumba pamoja na Magdalena Sakaya
kama mtu mwenye dhamana ya Katibu Mkuu wa CUF
Chama
Cha Wananchi (CUF) kipo katika mgogoro wa pande mbili upande wa Katibu
Mkuu wa CUF, Maalim Seif pamoja na upande wa Mwenyekiti wa CUF
anayetambuliwa na Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini Profesa Ibrahim
Lipumba, kufuatia mgogoro huo mpaka sasa kuna kesi mbalimbali ambazo
zimefunguliwa mahakamani kutokana na mvutano wa pande hizo zote mbili.
==>Hapo chini ni barua ya msaili wa vyama akijibu bara ya Maalim Seif
Post a Comment