MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR' YAONGOZA KITAIFA MCHEZO WA WANAFUNZI WASIOONA { GOLBO}
Mmoja
wa wanafunzi akikabidhi tuzo ya kombe ambalo walipata kuchukua ushindi
kwa Meya wa manispaa ya ilala jijini Dar hivi leo wa kwanza kushoto ni
Naibu meya wa manispaa hiyo Omary kumbilamoto,pamoja na Afisa elimu
Msingi wa Manispaa hiyo Bi Elizabeth Thomasi na aneyefuata ni katibu
tawala wa manispaa hiyo Edward Mpogolo
Mmoja
wa waalimu ambae amekuwa ni mlezi wa wanafunzi huo akikabidhi zawadi ya
Tuzo ya kombe kwa Meya wa manispaa ya ilala jijini Dar es salaam
Zawadi za Kombe zikiendelewa kukabidhiwa kwa manispaa hiyo ya ilala likiendelea
Haya ndiyo makombe yaliyokabidhiwa kwa manispaa ya ilala kama yanavyoonekanawa
kwanza kushoto ni Naibu meya wa manispaa hiyo Omary kumbilamoto,wa pili
kushoto ni Meya wa manispaa hiyo pamoja na Afisa elimu Msingi wa
Manispaa hiyo Bi Elizabeth Thomasi na aneyefuata ni katibu tawala wa
manispaa hiyo Edward Mpogolo
Baadhi ya waalimu pamoja na wanfunzi wakifurahia mara baada ya kukabidhi makombe hayo kwa manispaa ya ilala
Hawa
ni baadhi ya madiwani pamoja na watendaji mbalimbali walipo katika
ukumbi wa mikutano kwa ajili ya kikao chao cha baraza kujadili maendeleo
ya wilaya wakishudia kukabidhiwa kwa makombe hayo kwa manispaa yao
Manispaa
ya ilala hivi leo imepokea tuzo za kombe toka kwa wanafunzi
waliofanya vyema katika mchezo wa GOLBO ukiwa ni mchezo maalumu kwa
ajili ya wanafunzi wenye ulemavu wa macho kutoka katika shule ya uhuru
mchanganyiko iliyopo katika manispaa ya ilala jijini Dar es salaam.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhi makombe kwa ajili ya wanafunzi hao waliofanya
vizuri katika mchezo huo Meya wa manispaa ya ilala Charles Kuyeko ambae
pia siku ya leo ndie mwenyekiti katika kikao kinachoendelea cha baraza
la madiwani wa manispaa hiyo amesema kuwa wao kama madiwani wa manispaa
ya ilala wanapenda kutoa pongezi nyingi hasa kwa wanafunzi,waalimu
pamoja na maocha wao wa kimchezo hasa kwa kuwa saidia wanafunzi hao hadi
kuweza kuinuka kidedea katika mashindano hayo.
Hakuishia
hapo bali alizidi kuisihi halmashauri nyingine pamoja na shule nyingi
za hapa nchini kuhakikisha wanaweka mbele zaidi swala la elimu kwa
wanafunzi kwani huwa saidia katika kuboresha utendaji wao wa kimasomo
hasa wanafunzi wenye uhitaji maalumu kutoachwa bali waendelezwe kwa
michezo mbalimbali kama hii waliyoweza kuiletea wilaya ya ilala ushindi.
Naye
Afisa Elimu msingi wa manispaa hiyo ambaye pia ni kaimu mkurugenzi kwa
niaba ya mkurugenzi wa ilala amesema katika mipango yake ya awamu hii
kwa manispaa ya ilala ni katika kuhakikisha anaweka wigo mpana zaidi wa
kielimu pamoja na kuhakikisha sekta ya uwajibikaji kwa watumishi wote
ngazi ya elimu msingi kwa manispaa hiyo watajitahidi kufanikisha swala
la elimu bora michezo bora pamoja na uwajibikaji bora kwa utendaji wa
kiwilaya.
Huku
akitoa ufafanuzi kwa mchezo huo wa GOLBO kwa wanafunzi hao wasioona kwa
kusema huwa wanakuwa na mipira yao muhimu ambayo kwa ndani inakuwa na
kengele hivyo mwanafunzi anapokuwa anacheza husikiliza mlio wa kengele
na kufahamu ni wapi unapoelekea mpira huo.
Mchezo
huo ambao pia wanafunzi hao walipata kucheza na wachezaji kutoka timu
ya Everton pindi walipofika hapa nchini na kuamua kufanya ziara yas
kutembelea katika shule ya wanafunzi wenye ulemavu maalumu wa shule ya
uhuru mchanganyiko na kuonyesha umahiri wao.
Post a Comment