MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR' YAONGOZA KITAIFA MCHEZO WA WANAFUNZI WASIOONA {GOLBO}

Mmoja wa wanafunzi akikabidhi  kikombe cha  ushindi kwa Meya wa manispaa ya ilala jijini Dar hivi leo wa kwanza kushoto ni Naibu meya wa manispaa hiyo Omary kumbilamoto,pamoja na Afisa elimu Msingi wa Manispaa hiyo Bi Elizabeth Thomasi, na aneyefuata ni katibu tawala wa wilaya ya ilala Edwa Bw. Edward Mpogolo

Mmoja wa waalimu ambaye amekuwa ni mlezi wa wanafunzi huo akikabidhi zawadi ya  kikombe kwa Meya wa manispaa ya ilala jijini Dar es salaam
           Vikombe vikiendelea  kukabidhiwa kwa manispaa hiyo ya ilala
 Hivi ndivyo vikombe vilivyokabidhiwa kwa manispaa ya ilala kama yanavyoonekana wa kwanza kushoto ni Naibu meya wa manispaa hiyo Omary kumbilamoto,wa pili kushoto ni Meya wa manispaa hiyo pamoja na Afisa elimu  Msingi wa Manispaa hiyo Bi Elizabeth Thomasi na aneyefuata ni katibu tawala wa wilaya  Edward Mpogolo.

Baadhi ya waalimu pamoja na wanfunzi wakifurahi mara baada ya kukabidhi vikombe hivyo kwa manispaa ya ilala
 Hawa ni baadhi ya madiwani pamoja na watendaji mbalimbali walipo katika ukumbi wa mkutano kwa ajili ya kikao chao cha baraza kujadili maendeleo ya manispaa yao, wakishudia kukabidhiwa kwa makombe hayo kwa manispaa ya hiyo.(PICHA ZOTE NA JAMALI JAMALI UTOUH NEWS&Tv online)

                         TANZANITE BLOG

Manispaa ya ilala hivi leo imepokea jumla ya  vikombe nane(8) kutoka  kwa wanafunzi waliofanya vyema katika mchezo wa GOLBO ukiwa ni mchezo maalumu kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu wa macho kutoka katika shule ya uhuru mchanganyiko, iliyopo katika manispaa ya ilala jijini Dar es salaam.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa vikombe hivyo, kwa ajili ya wanafunzi hao waliofanya vizuri katika mchezo huo, Meya wa manispaa ya ilala Charles Kuyeko ambaye pia siku ya leo ndiye mwenyekiti katika kikao kinachoendelea cha baraza la madiwani wa manispaa hiyo, amesema kuwa wao kama madiwani wa manispaa ya ilala wanapenda kutoa pongezi nyingi hasa kwa wanafunzi,waalimu pamoja na makocha wao wa michezo, hasa kwa kuwasaidia wanafunzi hao hadi kuweza kuinuka kidedea katika mashindano hayo.

Hakuishia hapo  alizidi kuisihi halmashauri nyingine pamoja na shule nyingine za hapa nchini kuhakikisha kuwa wanaweka mbele zaidi swala la elimu, kwa wanafunzi kwani huwa saidia katika kuboresha utendaji wao wa kimasomo hasa wanafunzi wenye uhitaji maalumu kutoachwa bali waendelezwe kwa michezo mbalimbali kama hii waliyoweza kuiletea wilaya ya ilala ushindi.

Naye Afisa Elimu msingi wa manispaa hiyo ambaye pia siku ya leo katika kikao cha baraza la madiwani kinachoendelea  katika manispaa hiyo amechukua nafasi ya kaimu mkurugenzi kwa niaba ya mkurugenzi wa ilala amezungumza na kusema katika mipango yake ya awamu hii kwa manispaa ya ilala ni katika kuhakikisha anaweka wigo mpana zaidi wa kielimu pamoja na kuhakikisha sekta ya uwajibikaji kwa watumishi wote ngazi ya elimu msingi kwa manispaa hiyo watajitahidi kufanikisha swala la elimu bora michezo bora, pamoja na uwajibikaji bora kwa utendaji wa kiwilaya.

Huku akitoa ufafanuzi kwa mchezo huo wa GOLBO kwa wanafunzi hao wasioona kwa kusema huwa wanakuwa na mipira yao muhimu ambayo kwa ndani inakuwa na kengele hivyo mwanafunzi anapokuwa anacheza husikiliza mlio wa kengele na kufahamu ni wapi unapoelekea mpira huo
Mchezo huo ambao pia wanafunzi hao walipata kucheza na wachezaji kutoka timu ya Everton pindi walipofika hapa nchini na kuamua kufanya ziara yas kutembelea katika shule ya wanafunzi wenye ulemavu maalumu  wa shule ya uhuru mchanganyiko na kuonyesha umahiri wao.