Kesi ya Halima Mdee yapigwa kalenda.

Halima Mdee
Mbunge wa Jimbo la Kawe

Kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu chini ya Hakimu Victoria Nongwa imemuachia Mbunge Halima Mdee kwa Dhamana ya ahadi ya Shilingi 10 kwa kwa kila mdhamini mmoja, pamoja ambapo Wadhamini wake walikuwa wawili.

Kesi namba 218 ya 2017 ya kutumia lugha ya matusi, inayomkabili Mbunge wa kawe Halima Mdee imeahirishwa mpaka tarehe 12/20/2017 baada ya Hakimu Victoria Nongwa ambaye kesi hiyo iko chini yake kutokuwepo.

Julai 10, Halima aliesomewa shitaka la kutumia lugha ya matusi Dhidi ya Rais Magufuli "Rais anaongea Hovyo, "Afungwe Breki" Hata hivyo alipoulizwa kama nikweli Mdee alikana shitaka hilo.

Mbunge wa Jimbo la Kawe Halima Mdee alifikishwa katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu Julai 10, 2017 Jijini Dar es salaam majira ya Asubuhi.

 Halima Mdee (Chadema), alikamatwa Julai 4 Jioni, 2017, na Jeshi la Polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni Dsm kwa agizo la Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi. Kwa kile kilichodaiwa alitoa lugha ya kumtukana Rais Magufuli.