BANDA LA LA MANISPAA YA ILALA KATIKA MAONYESHO YA WAKULIMA NANE NANE KANDA YA MASHARIKI MJINI MOROGGORO LA FUNIKA, WENGI WALIMWAGIA SIFA.

Mkuu wa wilaya ya ilala Jijini Dar es salaam pamoja na Meya wa manispaa hiyo wakipokea maelekezo kutoka kwa mkulima wa asali alifika katika maonyesho ya nanenane yanayofanyika katika mkoa wa Morogoro kwenye viwanja vya nane nane

Mkuu wa wilaya ya ilala Bi sofia Mjema akiweka saini katika kitabu cha wageni mara alipofunga safari kutoka Dar es salaam hadi katika banda lao la maonyesho lililopo Mkoani morogoro kwa ajili ya kushiriki katika zoezi la ufunguzi wa maonyesho ya 26 ya maonyesho ya wakulima leo hii maoyesho haya ya wakulima kitaifa yanataraji kufanyika katika mkoa wa Lindi lakini kikanda ya mashariki yamefanyika katika mkoa wa morogoro.
 Wakwanza kushoto ni waziri wa maliaasili na utalii ambae ni amekuwa ni mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonyesho ya 26 ya nane nane akipata maelekezo toka kwa mkuu wa wilaya ya ilala na wa kwanza kulia ni mkuu wa mkoa huo wa Morogoro waote mara walipofika katika banda la ilala kwa ajili ya kujionea na kujifunza.

Hapa wote wakifurahia maonyesho hayo wakiwa pamoja na meya wa manispaa ya ilala mapema leo tarehe 01.08.2017


Hapa maonyesho yakiendelea

Banda lenye sungura ambapo kwa anaefika katika maonysho hayo hupata fursa ya kujifunza namna ya ufugaji wa sungura pamoja na kuelezwa mambo mengi yanayohusu ufugaji huo wa sungura

Hapa wakiendelea kupata maelekezo toka kwa mfugaji wa samaki juu ya namna gani ya kuwa na ufugaji bora wa samki ili uweze kupata faida kwa haraka zaidi yote haya ni katika banda la maonyesho ya ilala

                                
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo hii mara baada ya kufika katika banda la maonyesho kwa wilaya lililopo katika manispaa ya morogoro  Mkuu wa wilaya ya ilala Bi Sofia Mjema amesema Anatambua umuhimu na mchango mkubwa unaotolewa na wana ilala katika kuhakikisha wanafanikisha zoezi zima la maonysho hayo ya wakulima ya nane nane ambayo yameanza kuanzia hivi leo tarehe moja mwezi wa nane huku kilele chake kikitarajiwa kufika kilele ifikapo tarehe 08.08.2017

Ambapo amepongeza pia wote waliofika mapema pamoja na kuwa wa kwanza katika kuhakikisha wamefanikisha zoezi zima la maonyesho hayo ya wakulima yaliyopata kufunguliwa hivi leo na waziri wa maliasili na utalii Prof.Jumanne Magembe

Hakuishia hapo bali aliendelea kwa kusema lengo lake ni katika kuhakikisha anaisaidia wilaya ya ilala ili iweze kupata tuzo katika ubora na ushiriki wa maonyesho hayo kikanda na hiyo ndiyo itakuwa furaha kwake na kiwilaya nzima 

Hata hivyo katika banda hilo la maonyesho ya wakulima lilolokuwa limepambwa na maonyesho ya wakulimA mbali mbali ambao wote ni wakazi na wazawa wa manispaa hiyo ya ilala kutoka jinini Dar es salaam waliweza kupamba maonysho hayo kwa maonyesho mbali mbali kama vile mkulima akifika katika banda atapata kujifunza namna ya kujua na kufahamu juu ya ufugwaji wa samaki,mboga mboga,ulimaji wa uyoga ufugaji wa ng'ombe wa maziwa ufugaji wa kuku na namna nzuri ya utunzwaji wake pamoja na mambo mengi utakayojifunza pindi uingiapo katika banda lao la maonyesho ya nane Morogoro