WAKENYA WATATU WAHUKUMIWA KIFO KWA KUMVUA MWANAMKE NGUO
Mahakama moja ya Nairobi, siku ya Jumatano iliwahukumu wanaume watatu
kunyongwa, baada ya kupatikana na hatia ya kumvua nguo mwanamke mmoja,
kumdhalilisha na kujaribu kumbaka.
Kisa hicho kiltokea wakati wa wimbi la uvamizi wa wanawake miaka
mitatu iliyopita, ambapo makundi ya watu yalikuwa yakidai kwamba
wanawake walikuwa wanavaa mavazi yasiyokubalika.
Watu hao watatu walipatikana nahatia ya wizi wa kutumia nguvu, ambao hukumu yake ni kifo.
Hata haivyo, sheria ya hukumu ya kunyongwa nchini Kenya
haijatekelezwa tangu mwaka wa 1987, na hukumu kama hizo zimebadilishwa
na kuwa vifungo vya maisha.
Baadhi ya visa vya uvamizi huo, ambavyo vilikithiri mnamo mwaka wa
2014 vilirekodiwa kwanye simu za mkono, na kupelekea maandamano, huku
waliokuwa wakipinga vitendo hivyo - wengi wao wakiwa wanawake -
wakianzisha hashtag iliyoitwa #MyDressMyChoice kwenye mitrandao ya
kijamii.
Muathiriwa huyo aliiambia mahakama kwamba wanaume hao watatu walikuwa
kati ya kundi la wanaume saba waliotaka kumbaka ndani ya basi, lakini
wakakaachana naye alipowaambia kwamba alikuwa na virusi vya ukimwi.
Post a Comment