TRUMP ASHUTUMU UFICHUZI WA RIPORT DHIDI YA MWANASHERIA MKUU

Rais Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump ameishutumu ripoti iliofichuliwa kinyume cha sheria kwamba mwanasheria wake mkuu alijadili maswala ya kampeni na mjumbe mmoja wa Urusi.
Gazeti la Washington Post lilitoa maelezo kuhusu mikutano ambayo mwanasheria mkuu Jeff Sessions alifanya na balozi wa Urusi nchini Marekani Sergey Kislyak.
Bwana Sessions awali alikuwa amekana kufanya mazungumzo hayo kuhusu kampeni.
Mamlaka ya Marekani inachunguza kuhusu hatua ya Urusi kuingilia kati uchaguzi huo.
Huduma ya kijasusi inaamini kwamba Urusi iliingilia uchaguzi huo ili kumsaidia Trump kushinda .
Urusi imekana na Trump anasema kuwa kampeni yake haikushirikiana na Urusi.
Mmoja ya wale walionukuliwa anasema kuwa bwana Kislyak alizungumza na Sessions kuhusu maswala muhimu ya kampeni ikiwemo msimamo wa Trump kuhusu sera muhimu za Urusi.
Wakati alipothibitishwa mapema mwaka huu, bwana Sessions alisema kuwa hajawasiliana na Urusi wakati wa kampeni za uchaguzi.
Wakati ilipobainika aliwasiliana alisema kuwa swala la kampeni halikuangaziwa katika mkutano huo.