Mbunge wa Mkuranga kufunga Tamasha la SHIWATA.


index 
TAMASHA la Sanaa na Michezo la Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA)linaanza kesho Ijumaa jijini Dar es Salaam ambako wasanii zaidi ya 600 wanatarajia kushiriki.
Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa SHIWATA,Cassim Taalib na kuongeza kuwa mgeni rasmi atakayegungua semina hiyo ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Godfrey Mngereza.
Taalib alisema Mngereza atashuhudia michezo mbalimbali itakayoneshwa na wasanii na
  wanamichezo na Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega atafunga tamasha hilo Jumamosi.
  Alisema tamasha hilo ambalo awali lilikuwa lifanyike kijiji cha Wasanii
Mkuranga limehamishiwa jijini Dar es Salaam sababu kubwa ya kuhamisha
  tamasha hilo ni kutokana na mvua ya msimu uliopita kuharibu barabara ya
kwenda kijijini.

  Taalib alisema tamasha hilo sasa  litafanyika kwa siku mbili kuanzia kesho Ijumaa Julai 14.7.2017 na kuhitimishwa Jumamosi Julai 15 mwaka huu katika
  viwanja vya Chuo cha Uhazili, splendid Ilala Bungoni.
  Alisema mpaka sasa wameanza kupokea wanamichezo kutoka sehemu
mbalimbali kama vile Mkuranga, Kibiti, Zanzibar na Morogoro ambao washiriki tamasha hilo.
  Baadhi ya michezo ambayo itafanyika ni sarakasi, Tae kwon-do, muziki
  wa dansi, ngumi, soka,rede,muziki wa asili,wu shuu,ngoma,singeli na michezo
  mingine.
  Alisema kampuni ya SBC wanaotengeneza soda za Pepsi ndiyo
wadhamini wakuu wa tamasha hilo na kuongeza kuwa milango iko wazi kwa
  wadhamini wengine kujitokeza.
Akizungumzia ujenzi wa nyumba zao kijijini alisema mgawo na
  makabidhiano ya nyumba 14 ndogo,kubwa tatu na viwanja 35 vilivyopimwa
  utafanyika Julai 16 siku moja baada ya kumalizika tamasha hilo.
  Alisema kuanzia sasa wanachama wanaotaka kujenga nyumba zao wenyewe
  wawasiliane na Shiwata ili wapewe maelekezo na utaratibu wa kufanya usafi
kwenye makazi yao.
Mwenyekiti alisema utaratibu wa kulipia umeme kupitia mpango wa umeme
  vijiijini (REA)unaendelea na mikakati ya kukarabati barabara ya kufika
  kijijini unafanyika.