Chama cha ADC chawakingia kifua wafanyabiashara wa mafuta
Chama Cha Alliance for Democratic
Change (ADC) imeitaka Mamlaka ya Mapato nchini TRA kusitisha zoezi la
kuvifungia vituo vya mafuta nchini kwa kuwa limewakosesha huduma
watanzania wengi ambao kimsingi hawana hatia na hadha wanayoipata.
Akizungumza jana Jijini Dar es Salaam,
Katibu Mkuu ADC, Doyo Hassan Doyo, alisema kuwa ni vyema serikali
ikawachukulia hatua za kisheria wamiliki wa vituo hivyo vya mafuta na
kuruhusu huduma ziendelee kwani huduma ya mafuta imeendelea kuwa tatizo
kwa wananchi wa maeneo mbalimbali nchini.
“Mamlaka ya Mapato nchini ipo
katika oparesheni ya kuvifungia vituo vya mafuta nchini ambazo
havijafunga mashine za EFD katika ‘Pump ‘ za mafuta jambo ambalo
halichochei ukusanywaji wa mapato wenye ukweli wa takwimu,” alisema.
Katika hatua nyingine, Doyo alisema ADC
inakitaka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kutoingilia Mgogoro
ulikuwepo Ndani ya Chama cha Wananchi CUF.Ambapo amesema kuwa Chadema
kuingilia Mgororo wa CUF kunaweza kuhatarisha amani ya nchi.
Hata hivyo Doyo ameitaka serikali iviache vyama vya siasa nchini vifanye shughuli zao.
ADC ipo katika maandalizi ya
Maadhimisho ya kuzaliwa kwa Chama hicho ambayo yatafanyika Tarehe 22
Agosti Mwaka Huu ambapo chama hicho kitakuwa na ziara kwenye asasi za
Kiraia, kuwatembea Wagonjwa, Wafungwa, Vyuo vikuu na Kutembea Nyerere
Foundation ,N.K na Mwisho kuhitimisha kwenye Ofisi za chama hicho
Buguruni Jijini Dar es Salaam, huku vyama mbalimbali vikialikwa.
Post a Comment