Tanzania yaidhinisha rasmi matumizi ya dawa za asili kutibu nguvu za kiume.

Dawa za asili maarufu kama 'miti shamba'

Hivi karibuni nchini Tanzania kumeshamiri kwa uwepo wa matangazo mbalimbali ambayo mengine ni rasmi na mengine sio rasmi kuhusiana na dawa za asili haswa za kuongeza nguvu za kiume lakini sasa serikali ya nchi hiyo imethibitisha matumizi ya dawa tano za asili.
Huku miongoni mwa dawa hizo ni dawa ya 'Ujana' ambayo kazi yake ni kusaidia kuongeza nguvu za kiume wakati dawa nyingine zikiwa Sudhi, Vatari, IH Moon na Coloidal Silver ambazo kazi yake ni kukemea vimelea mbalimbali
Dawa za kiume za vidonge maarufu, ViagraHaki miliki ya pichaPA
Image captionDawa za kiume za vidonge maarufu, Viagra
DAWA ZA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME ZAWAPONZA WATU ZAMBIA
Baraza la dawa nchini humo limesema hatua hii imekuja baada ya uchunguzi wa kina uliofanywa na kubaini kuwa dawa hizo hazina madhara kwa afya ya binadamu hivyo hawana budi kuzikubali.
Aidha Paul Muhame ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa dawa za asili nchini Tanzania anasema baada ya baraza kupitisha vigezo vyote vilivyohitajika kutoka katika dawa hizo na mamlaka ya dawa na chakula wamethibitisha hilo.
"Suala la muhimu ambalo tumeliangalia zaidi ni usalama wa mtumiaji lakini katika upande wa kuthibitisha kuwa dawa hizo zinaponyesha au la ,linabaki kwa mnunuaji na mtumiaji wa dawa hiyo''.
Aina ya kuvu fulani nchini Nepal inayotambuliwa kwa uwezo wake wa kuongeza nguvu za kiume.
Image captionAina ya kuvu fulani nchini Nepal inayotambuliwa kwa uwezo wake wa kuongeza nguvu za kiume.
Aliongeza kwa kusema kwamba jukumu lao zaidi ni kuangalia usalama lakini sio dawa inatibu kwa kiwango gani.