WADAU WA ELIMU KUTOA ZAWADI KWA WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA WEEK YA ELIMU.
Mwanafunzi aliyeshika nafasi ya kwanza katika matokeo darasa la saba mkoa wa Dar es Salaam akipatiwa Zawadi. |
Katibu tawala Mkoa Theresa Mmbando,akikagua maonyesho mbalimbali kutoka katika shule tofauti. |
Wadau wa elimu wametakiwa kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha mazingira ya kazi za ufundishaji na ujifunzaji katika sekta ya Elimu,lengo likiwa ni kuinua na kukuza elimu kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa leo na Katibu tawala Mkoa Theresia Mmbando alipokuwa akizungumza katika hafla ya kuazimisha wiki ya Jukwaa la Elimu kwa mkoa wa Dar es Salaam,sambamba na tukio la kutoa tuzo na zawadi kwa wanafunzi walioshika nafasi ya kwanza katika shule, ngazi ya Wilaya na Mkoa kwa ujumla ambapo amwetoa wito kwa wadau wa elimu kuunga mkono jitihada na kushiriki vyema kuinua na kukuza sekta ya Elimu katika mkoani hapo, pia ameishukuru Serikali ya awamu ya tano chini Mh.Rais John Pombe Magufuli ambapo imehakikisha kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule anaandikishwa kupitia mpango wa elimu msingi bila malipo
"Tunaishikuru sana Serikali ya awamu ya tano kwa kuwa na dhamira ya dhati kwa kuhakikisha kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule anaandikishwa kupitia mpango wa elimu bure msingi bila malipo waraka wa elimu msingi 2016 umezingatiwa sana katika mkoa wetu ambapo tuanshudia ongezeko la usajili wa wanafunzi kwenye shule za umma kwa kila mwaka" Amesema Mmbando.
Tokea mwaka 2013 kiwango cha elimu kimeonekana kupanda ambapo ufaulu ulikuwa ni aslimia 75.19%,ambapo mkoa ulishika nafasi ya kwanza kati ya mikoa 25, mwaka 2014 ufaulu ulikuwa asilimia 78 %na mkoa ukashika nafasi ya kwanza kati ya mikoa 25, mwaka 2015 ufaulu ilikuwa asilimia 83.17%, ulishika nafasi ya pili kati ya mikoa 25, mwaka 2016 ufaulu ulikuwa asilimia 82.58%,ambapo ufaulu ulishuka kidogo na kupelekea kushika nafasi ya nne kati ya mikoa 26,na mwaka huu 2017 ufaulu ulikuwa ni asilimia 87.82% na kushika nafsi ya kwanza kati ya mikoa 26 na matokeo haya yametokana na ushirikiano kati ya wadau wa elimu na sekta ya elimu kwa ujumla.
Aidha katibu tawala mkoa amesema Serikali imeweza kutatua changamoto za miundo mbinu katika shule za msingi kwa kiasi katika mkoa huo, ambapo Mh. Rais Magufuli ameweza kuunga mkono kwa kutoa fedha zilizoweza kujenga vyumba vya madarasa matundu ya choo 14 pamoja na ofisi za walimu.
Vilevile ametoa pongezi kwa wadau wote wakiwemo walimu, wazazi pamoja na wafunzi waliofaulu na kuweza kuongoza katika shule na hata mkoa, ambapo amewataka wanaopokea tuzo hizo ziwe chachu kwa wote katika kuinua na kuunga mkono elimu katika mkoa huo.
Sambamba na hayo ametoa rai kwa watu na wadau mbalimbali kujitokeza kuchangia na kuunga mkono Sekta ya elimu katika kutatua changamoto mbalimbali ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi,wa mkoa wa Dar es Salaam.
Post a Comment