TEWUTA WAKINUKISHA KUHUSU AIRTEL, WATAKA IRUDISHWE SERIKALINI NA MALI ZOTE ZILIZOPORWA.

Chama cha wafanyakazi  cha Sekta ya Huduma za Mtandao wa  Mawasiliano  (TEWUTA)  kimeahidi kuunga mkono   Jitihada za Rais John Pombe Magufuli katika kufichua na kutafuta rasilimalia zote za nchi zilizopotea na kumilikiwa na taasisi au watu wachache kwa njia za kifisadi kwa manufaa yao binafsi.

Hayo yamesemwa leo na Katibu mkuu  Chama cha (TEWUTA) Junus Ndaro alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  leo jijini  Dar es Salaam, amabapo amasema chama chake kimepokea vyema agizo la Mh. Rais kupitia vyombo mbalimbali vya habari,kuhusu taarifa alizonazo zinazoonyesha kampuni ya AIRTEL ni Mali ya TTCL na kumwagiza Waziri wa Fedha kuanza uchunguzi na kubainisha ukweli wa jambo hilo.

"Kimsingi taarifa hii imewagusa watanzania walio wengi hususani wafanyakazi wa TTCL imekuwa faraja kubwa na furaha kwao kwa kuleta matumaini mapya na matarajio ya kushuhudia kampuni yao ya AIRTEL ambayo awali ilifahamika kwa jina(CELTEL) ikirejeshwa na kuwa mali ya Umma wa Watanzania baada ya kuporwa na viongozi wasio na Uzalendo"amesema Ndaro

Aidha amesema chama cha wafanyakazi TEWUTA wanampongeza Mh. Rais Magufuli  kwa kumwagiza Waziri wa Fedha kuanzanuchunguzi,utakaobainisha ukweli juu ya Ubinafiswaji wa TTCL na hatimaye kuanzishwa kwa kampuni ya simu ya CELTEL amabayo  ilitambuliwa pia kwa jina  la  ZAIN, Tanzania Ltd ambapo sasa ni AIRTEL.

Vilevile amesema wanatoa pongezi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi  kampuni ya  Simu Tanzania Omari Nundu, kwa kueleza Umma kupitia vyombo vya habari kuwa wako tayari kuthibitisha uhalali wa AIRTEL kuwa ni mali ya TTCL,ambapo chama cha TEWUTA wanaunga mkono .