Serikali mkoani Geita imejipanga kutatua kero ya maji kwa wananchi inayowakabili wananchi kwa muda mrefu.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel ametoa kauli hiyo alipotembelea miradi ya uzalishaji wa maji inayosimamiwa na Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jinni Geita, GEUWASA.
Alisema serikali imedhamiria kuona mji wa Geita unakuwa na maji ya kutosha ambapo kwa sasa kuna tanki lenye Mita za ujazo elfu moja na mia mbili na kwamba zipo jitihada za kuweka pampu itakayosaidia kuongeza maji kwenye tanki hilo ili kuweza kuongeza zaidi uzalishaji wa maji kwa maeneo ya mji huo.
Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshugulikia masuala ya Bonde la Ziwa Victoria Dr Ali Said Matano alisema mji wa Geita utanufaika na awamu ya tatu ya mradi wa maji kutoka Ziwa hilo kwa ufadhili wa Benki ya Afrika.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Geita, GEUWASA Bw Joseph Mwita amesema mahitaji ya maji mjini Geita ni Mita za ujazo 15 160 na kwamba maji yanayozalishwa ni Mita za ujazo kati ya 3 500 hadi 4000.
Post a Comment