RC MAKONDA ATANGAZA DISCOUNT YA 20% HADI 70% KWA WANANCHI WOTE WATAKAOFIKA MADUKA YA MLIMANI CITY.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. PAUL MAKONDA ametangaza Punguzo la Bei (Discount) la 70% kwa Bidhaa zote zinazopatikana Ndani ya Maduka Mlimani City kwa muda wa Wiki moja kuanzia Leo. 

Punguzo hilo la bei ni kwa Wananchi Wote ikiwa ni zawadi ya RC MAKONDA Kuelekea Sikukuu za Christmas na Mwaka Mpya ili kuwapunguzia Wananchi makali ya Garama.

RC MAKONDA amesema hayo kwenye Hafla ya kuwakaribisha wanafunzi wa Vyuo vikuu Mwaka wa Kwanza DAR FRESHERS PARTY 2017 ambapo amesema tamasha hilo litakuwa likifanyika kila Mwaka kwa kushirikisha Wasanii wakubwa kutoka Ndani na Nje ya Nchi. 

Ameshukuru Vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo TBC, E. FM na E TV pamoja na Channel Ten kwa kufanikisha Tamasha hilo. 

Aidha amewashukuru wasanii mbalimbali wakiwemo WCB, AY, FID Q,  RUBY, KASSIM MGANGA, MWANA FA,  RAY C, LADY JAYDEE, MSAMI, CHRISTIAN BELLA, DULY SYKES na MRISHO MPOTO kwa kujitolea kutoa Burudani bila Malipo.

Amesema Lengo la Tamasha hilo ni kujenga umoja kwa kuwakutanisha wanafunzi wa Vyuo mbalimbali kubadilishana mawazo  na kupatiwa maarifa.