Rais wa TFF ateuliwa ndani ya CECAFA
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ameshinda nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji katika Baraza la Soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Katika uchaguzi huo uliofanyika leo Desemba 2, 2017 jijini Nairobi, Kenya Rais Karia alipita bila kupingwa baada ya wanachama watatu kati ya nane kujitoa hivyo watano waliobaki kuchaguliwa bila kupingwa.
Wajumbe hao ambao wataungana na Rais wa CECAFA, Mhandisi Mutasim Gafar wa Sudan watakuwa na kibarua cha kuboresha utendaji kazi wa baraza hilo kwa ajili ya kuimarisha soka la Afrika Mashariki na kati.
Wengine waliochaguliwa ni Abdiqaani Arab Said (Somalia), Aimable Habimana (Burundi), Juneid Basha Tilmo (Ethiopia) na Mwanamke Petra Dorris wa Kenya.
Post a Comment