Mkurugenzi Mtendaji CRDB kuachia ngazi
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei ametangaza kutoongeza mkataba pindi mkataba wake wa sasa utakapomalizika Mei 31, 2019.
Akiongea leo Dkt. Kimei amesema ameamua kutoongeza mkataba hivyo anatoa nafasi kwa mchakato wa kumtafuta mrithi wake uanze kama ambavyo sera ya Benki hiyo inaeleza.
“Nimeamua kutoongeza muda wangu wa mkataba mara tu mkataba huu nilionao sasa hivi utakapoisha, mkataba wangu unamalizika Mei 31, 2019 ambapo ni takribani miezi 17 kabla, na sera ya Benki inasema mchakato wa kumpata mrithi wa Mkurugenzi Mtendaji lazima uanze miezi 18 kabla ya aliyepo kumaliza muda wake”, amesema Kimei.
Aidha Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa Bodi ya Benki hiyo itaanza mchakato wa kumpata mrithi wake mapema mwezi Januari, zoezi ambalo litakamilika ifikapo Mei, 2019 kabla ya yeye kukabidhi kijiti hicho.
Dkt. Kimei amekaa kwenye nafasi hiyo kwa miaka 20 na atakamilisha miaka 21, Mei 31 2019 atakapokuwa anastaafu rasmi na kumwachia nafasi Mkurugenzi mpya atakayepitishwa na bodi baada ya mchakato wa miezi 17.
Post a Comment