MKOA WA DAR ES SALAAM KUONGOZA KATIKA MATOKEO YA DARASA LA SABA.


Mkoa wa Dar es Salaam,umetangangaza kutakuwepo na wanafunzi wa  chaguo la pili katika matokeo ya darasa la saba na badala yake wanafunzi wote wamepangiwa shule moja kwa moja hii ni baadae ya kupata ufaulu mzuri na kuongoza kitaifa
Akizungumza katika Kikao cha uchaguzi wa wanafunzi kidato cha kwanza 2018/wa mkoa huo , Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Katibu Tawala mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando amesema   katika matokeo ya Darasa la saba mwaka huu wanafunzi wote 58,573 walifanya vizuri sawa na asilimia 87.82%  ukilinganisha na mwaka 2016/ambapo wanafunzi wote wamepangiwa shule na Wataanza kidato cha kwanza January  8,2018.
Katibu tawala Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni mwenyekiti wa kikao cha uchaguzi wanafunzi kidato cha kwanza kwa mwaka 2018 Theresia Mmbando akizungumza katika mkutano huo.

afisa Elimu mkoa wa Dar es Salaam, Hamis Lissu(kulia) akitambulisha  wajumbe waliofika katika kikao hicho.


Amesema, wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na shule za  ufaulu mzuri zaidi  ni 68,  wavulana 35 na wasichana 33,na Wanafunzi waliochaguliwa  shule za ufundi ni 74,wavulana 68 na wasichana 6,shule za bweni kawaida  ni 24 wavulana 12 na wasichana 12
Amesema,  wanafunzi 1,931 wamechaguliwa kujiunga na shule za Sekondari zinazo chukua wanafunzi wa mkoa wa Dar es Salaam, ambapo wavulana ni 850 na wasichana 1, 081.
Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga katika shule za serikali za wananchi ni 56,299 ikiwemo wavulana 27,035 na wasichana 29,264 huku wanafunzi wenye uhitaji maalum waliopangiwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI ni 101 wavulana wakiwa ni 58 na wasichana 43.

Amefafanua kuwa, waliochaguliwa Manispaa ya Ilala ni wanafunzi 19,236,kigamboni 2,803,Kinondon 10,885  Temeke15, 323na Ubungo ni 10,326.

Vilevile Jumla ya  nafasi 4,685 katika shule za pembezoni mwa jiji zimebaki wazi kwa sababu ya umbali uliopo kati ya shule ya msingi waliposoma wanafunzi na mahali shule zilipo, nafasi zizo baki kwa Manispaa ya Ilala ya Ilala (mjini) ni 887,kigamboni590, Kinondon 1,718 na Ubungo 1,490.

Amesema asilimia,   wanafunzi waliojiunga na shule za  secondari kwa waliofanya mtihani kwa mkoa ni asilimia 87.82%. katika Manispaa ya Ilala (mjini) ni asilimia 92.48.Ilala (Vijijini) asilimia 84.42.Manispaa ya Kinondoni 93.02%Temeke 81.74%.Kigamboni 91.10% na Ubungo ni 89.01.

Aidha Mmbando amewataka wazazi na walezi wa wanafunzi kuwapeleka watoto wao shule waliopangiwa   January 8,2018 bila kukosa, na kuwakumbusha wakuu wa shule 147 zinazo pokea wanafunzi kuzingatia waraka no 2 wa 2016 unaohusu uendeshaji wa elimu bure bila malipo.