Marufuku kulazimisha kodi ya mwaka - Lukuvi
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, amewataka wamiliki wa nyumba nchini kuwapa fursa wapangaji kulipa kodi ya mwezi mmoja mmoja badala ya miezi sita au mwaka.
Waziri Lukuvi ameyasema hayo leo Desemba 5, wakati akifungua jengo la ofisi ya makao makuu ya shirika la nyumba nchini (NHC).
“Mpangaji anatakiwa kulipa kodi kila mwezi labda awe ametaka mwenyewe kulipa miezi sita au mwaka kama uwezo wake unaruhusu kufanya hivyo”, amesema Lukuvi.
Lukuvi amesisitiza kuwa wamiliki wa nyumba kuanzia sasa wanatakiwa kulipwa kila mwezi, ili iwape fursa wapangaji kuwa na maisha yanayowezekana kuishi maeneo ya mjini.
"Acheni tamaa wenye nyumba, chukueni kodi kila mwezi" , amesema Lukuvi.
Hivi karibuni kumekuwepo na mjadala kuhusu namna ya kulipa kodi baada ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula kuweka wazi kuwa wizara hiyo iko mbioni kuja na sheria itakayomwezesha mpangaji kulipa kodi kwa mwezi mmoja mmoja.
Post a Comment