Majeshi ya Polisi Tanzania na Rwanda yaungana
Majeshi ya Polisi ya Tanzania na Rwanda yameunganisha nguvu kupitia Majeshi yao ya Polisi chini ya wakuu wake IGP Simon Sirro Tanzania na RNP Emmanuel Gassana wa Rwanda ili kupambana na uhalifu, ujangili na kuangalia namna ya kutatua matatizo.
yanayokumba nchi hizo.
Akizungumza na wanahabari leo akiwa Tanzania RNP Gassana amesema kuwa lengo ni kushirikiana kutokana na changamoto ambazo zinatokea katika nchi ikiwemo kuongeza nguvu, teknolojia, vifaa na kuongeza uzoefu wa matumizi ya vifaa.
Kwa upande wa Tanzania, IGP Sirro amesema kuwa kwa ushirikiano huo ambao unafanyika kwa kuangalia nini ambacho kinatakiwa kufanywa na maarifa ambayo yatatumiwa ili Jeshi la Polisi liweze kufanya kazi yake kwa usahihi na kupunguza uhalifu na endepo mtu akijiingiza kwenye uhalifu anaweza kupoteza familia yake na kuishia pabaya.
“Wenzetu Rwanda wako mbele katika matumizi ya teknolojia, hivyo kuna baadhi ya mambo ambayo watatuelekeza na tutapata uzoefu katika kupambana na wahalifu wa mitandaoni ambao wamekuwa wakiwasumbua raia. Sisi pia tuna uzoefu wa mambo mengi ambayo wenzetu Rwanda watajifunza kutoka kwetu,” amesema Sirro.
Post a Comment