Wachina wakamatwa nchini
Raia wanne wa kigeni wenye asili ya China wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kuendesha kiwanda cha kutengeneza mifuko ikiwemo ya plastiki kinyume na sheria huku kiwanda hicho kikitozwa faina ya shilingi Milioni 7 kwa makosa ya kisheria.
Akizungumzia kukamatwa kwa raia hao mara baada ya kufanya ziara katika kiwanda hicho leo jijini Dar es salaam Naibu waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde amesema raia hao wa kigeni wamekiuka taratibu na sheria za uendeshaji kiwanda kilichopo kwenye makazi ya watu na kuagiza kifungwe kwa muda ili kupisha uchunguzi wa usajili wake.
Amesema serikali inawapenda wawekezaji kwenye sekta ya viwanda waje kwa wingi kuwekeza nchini lakini ni lazima nao wafuate sheria za nchi katika uwekezaji wao
Post a Comment