VIONGOZI WENGINE IGENI MFANO WA MAKONDA:RAIS MAGUFULI
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania DR. JOHN MAGUFULI Leo ametembelea Meli ya Jeshi la China na kuaga Meli hiyo ambapo amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. PAUL MAKONDA kwa kufanikisha Ujio wa Meli hiyo.
Rais MAGUFULI amesema kuwa RC MAKONDA ni Kiongozi mwenye upendo na anaethamini Wananchi wake hivyo anapaswa kuigwa na Viongozi wengine.
Amesema utaratibu wa Upimaji wa Afya na Matibabu Bure ulioanzishwa na RC MAKONDA umesaidia kuokoa Maisha ya Wananchi wengi waliokuwa wakipoteza maisha kwa kushindwa kumudu garama za matibabu.
Aidha Rais MAGUFULI amempongeza RC MAKONDA kwa kampeni aliyoanzisha ya kutafuta Miguu ya Bandia kwa watu wenye uhitaji pamoja na kufanikiwa kutafuta Magodoro 1,000 kwaajili ya kuhakikisha Hakuna Mgonjwa anaelala Chini.
Pia Rais MAGUFULI amesifu ubunifu wa RC MAKONDA kwenye kufufua Magari yaliyokufa na kumtiat moyo kuwa aendelee kupiga Kazi
Post a Comment