*RC MAKONDA KUWAKARIBISHA WANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA KIZALENDO*.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa *PAUL MAKONDA* ameandaa tamasha la *kuwakaribisha Wanafunzi wa Mwaka wa kwanza kwa Vyuo Vikuu vya Mkoa wa Dar es Salaam* kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya *maendeleo, kuwaepusha kuingia kwenye makundi hatarishi.*
Tamasha hilo linalotaraji kufanyika eneo la Maegesho *Mliman City* litatawaliwa pia na *Burudani kutoka kwa Wasanii Mbalimbali* ambapo vyombo vya Habari vya *TBC, CHANNEL TEN NA E FM wamejitolea kulibeba tukio hilo la kipekee.*
*RC MAKONDA* amesema hayo Leo wakati wa Mkutano na hafla ya kupata Chai na *Maraisi wa Vyuo Vikuu vya Mkoa wa Dar es salaam pamoja na Viongozi wa Asasi za Kiraia.*
Katika Mkutano huo *Vyuo vikuu vimeunga Mkono kampeni ya ujenzi wa Ofisi za Walimu* kwa kuchangia Mifuko 25 ya Saruji na kuahidi kuendelea kuunga mkono kampeni hiyo.
Aidha *RC MAKONDA* ametoa nafasi kwa *Vyuo vikuu kumuweka kikaangoni* kwa kufanya mdahalo wa *kubadilishana mawazo* na kuelezana changamoto.
*RC MAKONDA* pia amesema anao mpango wa kuandaa *Shindano la Uongozi Wanafunzi wa Vyuo vikuu* kwa lengo la kuwajengea Wanafunzi uwezo wa uongozi bora na namna ya *kupatia majibu changamoto* ambapo Mshindi atapata ofa ya *kusoma Bure Chuo cha Diplomasia.*
Kwa upande wake *Kamanda wa Polisi* kanda Maalumu ya Dar es Salaam *LAZARO MAMBOSASA* amewaomba Wanafunzi wa vyuo vikuu *kutoa taarifa kwa jeshi la Polisi pale wanapobaini uwepo wa Wahalifu.*
Post a Comment