RC MAKONDA AKABIDHI MASHINE KUMI ZA ULTRA SOUND VITUO VYA AFYA, AJIPANGA KUUNDA KAMATI YA WANASHERIA WALIOBOBEA KUWASAIDIA WAKINAMAMA.
Bw.Yohana Kasalala |
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda anatarajia kuunda Kamati ya Wanasheria Waliobobea kwa ajili ya kuwasaidia wakinamama wanaopewa ujauzito na kukataliwa na wanaume zao na kusababisha kukosekana kwa huduma na malezi bora.
Akizungumza leo katika hafla ya kukabidhi Mashine za Ultra sound kwa vituo vya afya na hospitali 10 ambazo zimeonekana kutoa huduma bora za ya uzazi na mtoto.
Mhe. Makonda amesema kuwa baadhi ya wanaume wamekuwa wakiwatelekeza wakinamama baada ya kuwapa ujauzito bila kuwapa matuzo.
Kutoka kushoto ni Mganga Mkuu wa Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa, Mwakilishi wa CCBRT, Naibu Mstahiki Meya wa Ilala. |
“Kutakuwa na kamati ya wanasheria waliobobea pale ofisi kwangu ambao kazi yao itakuwa kuwasaidia wakinamama ambao wanaume zao wanashindwa kuwapa huduma muhimu” amesema Mhe.Makonda.
Mkuu wa Mkoa akitoa Mashine za Ultra sound kwa hospitali zilizofanya vizuri katika kutoa huduma afya ya uzazi na mtoto. |
Amefafanua kuwa wanaume hao watachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani ili kuhakikisha hatua za kisheria zinachukuliwa ili mama na mtoto wapate huduma hadi pale watakapoweza kujiudumia mwenyewe.
Katika hatua nyengine amewapongeza madaktari pamoja na wauguzi kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya kwa kupunguza changamoto katika vituo vya afya.
“Kazi ya yenu ni wito basi ni vema kutengeneze mazingira mazuri ili kazi ya wito ufanyike kikamilifu” amesema Mhe. Makonda.
Dkt. Brenda Sequeira D’mello akiwa katika hafla ya kutoa zawadi kwa hospital zilizofanya vizuri Mkoa wa Dar es Salaam. |
Ameeleza kuwa kazi ya serikali ni kuhakikisha hakuna mama wale mtoto ambaye anaweza kupoteza maisha na wataendelea kuboresha huduma za afya katika mkoa wa Dar es Salaam.
Meneja wa Uendeshaji katika mradi wa kutoa huduma ya Afya na Uzazi Shirika CCBRT Yohana Kasalala, amesema kwa kutambua umuhimu wa afya wameamua kuanzisha mashindanao ya utoaji huduma kwa mama na mtoto.
Amesema kuwa hospitali 22 zimeweza kushiriki katika mashindano hayo ambapo vituo kumi ndio vimeweza kuwa washindi na kupewa zawadi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda. |
Kasalala amefafanua kuwa vigezo vilivyotumika ni pamoja na kuangalia utendaji wa kazi ambao unatumika kila siku, utuzaji wa twakimu za mama na mtoto tangu anapojifungua.
Mshauri wa Kiufundi wa Mradi wa kujenga uwezo wa CCBRT Dkt. Brenda Sequeira D’mello, kitendo cha kuzipatia hospitali mashine ni sehemu ya utekelezaji wa mradi miaka saba wa kuwajengea uwezo watumishi wa afya na kuboresha miundombinu.
“Lengo ni kuhakikisha wanatoa huduma ya afya za uzazi na mtoto na wanakuwa na ujuzi unaohitajika na kuboresha miundombinu ya afya” amesema Sequeira D’mello
Hosiptali zilizofanikiiwa kufanya vizuri na kupewa zawadi ya mashine hizo ni pamoja na Vijibweni, Mbagala rangi tatu, Sinza, Temeke, Tandale, Kimara, Mnazi Mmoja, huku hospitali ya Amana ikifanikiwa kushika nafasi ya kwanza ikifatiwa na Mwananyamara
Post a Comment