*RC MAKONDA AANDIKA HISTORIA, MELI KUBWA YENYE HOSPITAL NDANI YAWASILI NA MADAKTARI BINGWA KUTOKA CHINA*

Meli kubwa ya Jeshi la Jamuhuri ya China yenye Hospital ndani *imewasili Leo ikiwa na Madaktari Bingwa 381,Vifaa na Madawa ya kutosha* kwaajili ya kuanza kwa zoezi la *Upimaji na Matibabu Bure* kwa wakazi wa Dar es Salaam. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam *Mhe. PAUL MAKONDA* ametembelea Meli hiyo na kujionea namna *imesheheni Vifaa tiba vya Kisasa* ambapo ndani yake vipo *vyumba 8 vya Upasuaji*, Vyumba vya *ICU, Wodi za Wagonjwa, Vyumba vya Madaktari, Mitambo ya kisasa, Mahabara na Sehemu ya Wagonjwa kupumzika.* 

Meli hiyo ya kipekee ina *Helicopter kwaajili ya wagonjwa* ambapo kwa Ulimwenguni *Meli za Aina hiyo zipo Mbili pekee* ambapo moja ni hii iliyokuja Tanzania na nyingine ipo *Nchini Marekani*.

RC MAKONDA  amesema Meli hiyo ina *mfumo maalumu wa Mawasiliano Kati ya Meli na Taifa la China* pale inapotokea Ugonjwa umeshindikana.
Tayari *Jopo la wataalamu 30 wameenda Hospital za Amana, Temeke, Mwananyamala na Ocean Road* kwaajili ya *kukarabati na kufunga vifaa vipya* kwa vile vitakavyobainika vilivyoharibika au Kufa. 
Amesema *lengo la Serikali ni kuhakikisha Hakuna mwananchi anaepoteza maisha kwa kigezo cha kukosa huduma.*

Amewasihi *Wananchi wenye magonjwa yaliyoshindikana kwa muda mrefu kuchangamkia Fursa hii ya matibabu Bure* chini ya Madaktari Bingwa kutoka China. 
Kwa upande wake kiongozi Mkuu wa Meli hiyo *Kamanda GUAN BAILIN* amesema *wamekuja na vifaa vya kutosha na madaktari waliobobea* hivyo wananchi Wajitokeze kwa wingi.