MUME WA IRENE UWOYA KUFARIKI DUNIA MAPEMA LEO HII

Aliyekuwa Mume wa zamani wa Muigizaji Irene Uwoya na Mchezaji wa Burundi, Hamadi Ndikumana Katauti amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Taarifa za kifo cha Ndikumana zimethibitishwa na Muigizaji Irene Uwoya ambaye alikuwa mke wake wa ndoa na kufanikiwa kuzaa mtoto mmoja wa kiume.
Baaada ya muda EATV ilifanikiwa kumpata Haruna Niyonzima ambaye ni moja ya watu wake wa karibu, na kusema kwamba chanzo cha kifo cha Ndikumana ni maumivu ya kichwa aliyoyapata ghafla alipotoka mazoezini jana jioni.
Ndikumana na Uwoya walifunga ndoa Julai 2009 jijini Dar es salaam katika kanisa la Mt. Joseph, na walitengana baada ya  muda mfupi.