MPIGAPICHA MKONGWE KUTOKA DENIMARK ,ALIYEPIGA PICHA TANZANIA MIAKO 50 ILIYOPITA KUFANYA ONESHO MAKUMBUSHO YA TAIFA.

Makumbusho ya taifa Tanzania,kwa kushirikiana na bwana Jesper Kirknaes kutoka Dernmark ,kwa udhamini wa ubalozi wa denmark nchini imeandaa onyesho la picha liitwalo"Karibu Tanzania"Kuuhusu kazi mbalimbali na maisha ya watanzania miaka 50 iliyopita.




Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Pro. Audax Mabula aliyepo katikati, aliye upande wa kushoto ni mpiga picha mkongwe kutoka Nchini Denmark Jester kirknaes


Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi mkuu wa makumbusho ya Taifa Prof:Audax Mabula,Amesema onyesho hili litafunguliwa rasmi na mheshimiwa balozi wa denmark nchini Einah .H.Jensen tarehe 16/11/2017 saa saba 7:00 mchana katika makumbusho ya taifa dar es salaam,Ambapo amesema mabalozi,viongozi mbalimbali na wananchi wanatarajiwa kuudhuria ufunguzi huo.






Amesema,Onyesho hili litahusisha maonyesho ya vifaa na picha mbalimbali zinazohusu maisha na kazi zilizokuwa zinafanywa an watanzania,na kufafanua kuwa nia ya kuweka onyesho hili ni kuonyesha uhalisia wa kazi na maisha ya watanzania miaka 50 iliyopita halia ambayo ingekuwa ni vigumu kuelezea kwa maneno






Sanjari na ,picha vionyeshwa halisi vitakuwepo ili kutoa fursa kwa watu kuona jinsi ilivyokuwa vinatengenezwa hatua kwa hatua mpaka kupata kifaa husika,picha hizo,zilipigwa mwanzoni mwa mwaka 1968 hadi mwaka 1977,amesema kuwa picha hizi zinaumuhimu mkubwa kihistoria na kiutamaduni kutokana na mabadiliko ambayo tunayoyaona sasa katka jamii zetu.


"Kwa mfano kila kabila lilikuwa na aina yao ya nyumba na walijitegemea vyombo vyao vya nyumbani kama vyungu,vikapu,nakadharika".






Hata hivyo,amesema katika wakati huu ambapo Tanzania , jnlekea kuwa na uchumi wa viwanda onyesho hili linatoa funzo kubwa kutokan na kwamba watanzania wenzetu ambao waliweza kuendesha maisha yao kujtengenezea vitu walivyovihitaji wenyewe katika ulimwengu wa sayansi na teknologia bado watanzania wanaweza kufanya mambo makubwa kuliko waliofanya miaka mingi iliyopita.






Pamoja na hayo,prof:Mabula amesema kuwa uwepo wa onyesho hili katika makumbusho ya taifa n sehemu sahihina amewataka watu kwenda kwa wingi kujionea wapi jamii ilikotoka na wapi inakokwenda.