Mgambo kuajiriwa na makampuni binafsi
Taarifa na Gasper Pascal
Wahitimu wa mafunzo ya mgambo mkoa wa Dar es Salaam wametakiwa kutumia mafunzo waliyoyapata, kwa kufanya shughuli za kizalendo na kuepuka kuwa chanzo cha uhalifu na maovu katika jamii.
Hayo yamesemwa leo na mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix lyaniva alipokuwa akifunga mafunzo ya Mgambo kundi la 55 lenye jumla ya washiriki 819 waliohitimu leo jijini Dar es Salaam ambapo amewataka kutumia mafunzo waliyoyapata kwa kuwa wazalendo na kufanya shughuli mbalimbali za ulinzi shirikishi katika jamii.
"Mafunzo mliyopata myatumie kwa kufanya shughuli mbalimbali za kizalendo kwa kuokoa maafa,Msiende kuwa chanzo cha Maovu na uhalifu huko mitaani wekeni Uzalendo mbele" Amesema Mh. lyaniva
Aidha amewapongeza washiriki wote waliohitimu mafunzo hayo ambapo amewataka washauri wa kila wilaya waweze kuwapatia barua watakayopeleka kwa mtendaji wa kila kata ili waweze kuwekwa kwenye Ulinzi shirikishi katika katika kila mtaa.
Vilevile ameongeza kuwa makampuni binafsi wanatakiwa kuchukua walinzi kwa kufuata taratibu na sheria ikiwa ni pamoja na kuonyesha mkataba wa kazi, utakaonyesha mshahara anaolipwa muhusika na kuuwasilisha kwa mshauri husika wa Jeshi la Akiba kwa kila wilaya lengo ikiwa ni kupata walinzi.
Katika hafla hiyo Mh Felix lyaniva amekagua gwaride la Mgambo hao, pamoja na kutoa vyeti kwa washiriki wa kila Washiriki wa kila wilaya, ambazo ni Ilala, Temeke, Kigamboni Ubungo na Kinondoni.
Katika hafla hiyo ya kufunga mafunzo ya Mgambo kikundi cha 55 washiriki waliohitimu mafunzo hayo wametoa maonyesho mbalimbali waliyoyapa kipindi chote cha mafunzo muda wa miezi minne ambapo wameonyesha, onyesho la mapigo ya kareti, Gwaride kupita mbele kwa mwendo wa pole na haraka Onyesho la kwata ya kimyakimya, pamoja na onyesho la Singe.
Kwa upande wake mshauri wa Jeshi la Akiba mkoa wa Dar es Salaam, Kanali Ismail amemshukuru Mhe: mgeni rasmi kwa kufika katika hafla hiyo na kufunga mafunzo hayo ambapo ameiomba serikali kuangalia changamoto za gharama ya mafunzo ambapo washiriki wanaopenda kujiunga na mafunzo na wanashindwa kumudu.
Post a Comment