MAKONDA ATANGAZA NEEMA YA AJIRA KWA MABAHARIA WAZAWA
HABARI NA GASPER PASCAL
Mkuu wa mkoa wa dar es Salaam Paul Makonda ameahidi kutatua changamoto zinazowakabili mabahari kwa lengo la kuwawezesha mabaharia kupata kazi ndani na nje ya nchi.
Makonda ameyasema hayo leo katika ufunguzi wa mkutano wa mabaharia na kusema changamoto hizi zikitatuliwa zitaweza kutatengeneza fursa ya watu kupata kazi, kuheshimika na usalama wa mwajiriwa, uhakika wa kazi pamoja na kufanya kazi kwa ufanisi.
"Naamini changamoto zote hizi ambazo nimeziona zipo kwenye makundi matatu ninaweza kuzitatua na tutaendelea kushirikiana na kuweka mikakati itayowawezesha mabaharia kunufaika, na niwahakikishie kwamba tutafanikiwa." Amesema
Aidha amebainisha kuwa zikitokea nafasi za kazi kwa mabaharia watapewa kipaumbele ili waweze kulinda vyema rasilimali za nchi na kuepusha kusafirisha Mali za magendo na kusaidia kukuza uchumi wa taifa kwa kuweza kulipa kodi kikamilifu.
Pia amezungumzia suala la.upimaji afya bure litakaloanza November 19, mwaka huu litakalofanywa na madktari kutoka China na watafanya huduma hiyo bure kwa Siku saba na kuwaambia mabaharia ni fursa kwao kuweza kupima afya kwa lengo la kuchukua taadhari mapema kabla ya tatizo kuwa kubwa.
"Nawataka wanachi wote wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kupima afya bure November 19 itakayotolewa na madktari 381,kutoka nchi ya china na ni fursa kwa ninyi mabaharia kupima afya zenu sitopenda kuona au kusikia Baharia au mkazi wa mkoa huu anaumwa ghafla tahadhari ni bora kuliko tuba". Amesema Makonda.
TAZAMA KWENYE VIDEO HII HAPA CHINI!
Post a Comment