Samson Mwigamba ajiuzulu

Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni na Uchaguzi Taifa ya Chama Cha ACT Wazalendo Samson Mwigamba ameng'atuka nafasi yake hiyo katika chama hicho na kubaki mwanachama wa kawaida kwa madai ya kuwa ameona kuna mambo ndani ya chama hicho hayaendi sawa.
Kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe alipokuwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni na Uchaguzi wa Taifa wa ACT- Wazalendo Samson Mwigamba.

Akiongea na East Africa Radio, Samson Mwigamba amedai kuwa amejitahidi sana kuongea na viongozi wakuu wa chama hicho kuhusu mambo mbalimbali lakini ameona yamekuwa hayatendeki wala kufanyiwa kazi hivyo ameamua kufanya maamuzi hayo ili kutokuwa pingana nao bali ameamua kubaki kama wanachama wa kawaidia ili aweze kupata nafasi ya kuhoji baadhi ya mambo ndani ya chama.