Samatta na Msuva wahitajika nyumbani
Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Salum Mayanga ametaja kikosi cha timu hiyo kitakachoingia kambini kwaajili ya mchezo wa kirafiki wa Kalenda ya FIFA inayoanza Novemba 6 hadi 14 mwaka huu
Mayanga amewataja makipa Aishi Manula, Peter Manyika na Ramadhani Kabwili kuunda kikosi hicho wakisaidiwa na mabeki ni Boniphace Maganga, Abdi Banda, Gadiel Michael, Kelvin Yondani, Nurdin Chona, Erasto Nyoni na Dickson Swai.
Kwenye orodha hiyo viungo ni Himid Mao, Hamis Abdallah, Mzamiru Yassin, Raphael Daudi, Simon Msuva, Shiza Kichuya, Ibrahim Ajib, Mohamed Issa, Farid Mussa na Abdul Mohamed.
Washambuliaji ni Mbwana Samatta, Mbaraka Yusuph, Elias Maguli na Yohana Mkomola.
Shirikisho la soka nchini TFF limekubaliana na timu ya taifa ya Benin kuwa ndio timu ambayo itacheza na Taifa Stars kwenye mchezo huo wa Kalenda ya FIFA Novemba 11.
Post a Comment