Odinga aanza kujishuku

Kiongozi wa Muungano wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga amesema Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume Huru wa Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ya nchini Kenya Ezra Chiloba bado yupo ofisini ingawa alisema kuwa amechukua likizo na asingeshiriki  katika uchaguzi.
Akizungumza Jumatatu katika mkutano wa kampeni ya kupambana na uchaguzi huko Keroka, kata ya Kisii, Raila amesema kuwa Chiloba amekwenda katika  ofisi hiyo asubuhi ya jana na kwamba mpaka muda ule aliokuwa akihutubia alikuwa bado anafanya kazi zake za tume ya uchaguzi.
"Ninawahakikishia kuwa leo asubuhi saa moja  asubuhi, Chiloba alikuwa katika ofisi yake, na bado yupo mpaka sasa alisema Raila.
Kiongozi huyo wa upinzani pia alisisitiza kuwa hakutakuwa na uchaguzi mnamo Oktoba 26 kama hali ya "kiwango cha chini" ambacho Chama cha muungano NASA ulikuwa unahitaji kuwa haujafikiwa na IEBC.
Kenya inatarajiwa kufanya uchaguzi wa Marudio Oktoba 26 siku ya Alhamisi baada ya ule uchaguzi mkuu uliofanyika Agust 08 kufutwa na Mahakama ya juu nchini humo kwa madai kwamba ulikuwa na dosari za kutosha.